
DAR ES SALAAM — Mshambuliaji Anicet Oura amekuwa shujaa wa Simba SC baada ya kufunga bao la ushindi katika dakika za lala salama na kuipa timu hiyo ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Simba SC ilianza mchezo huo kwa kasi na kupata bao la mapema dakika ya 3 kupitia kwa Oura, aliyetumia vyema nafasi hiyo kuifanya Wekundu wa Msimbazi kuongoza mapema. Hata hivyo, Namungo FC walirejea kwa kasi kipindi cha kwanza kupitia kwa Lulendi, aliyefunga mabao mawili mtawalia dakika ya 35 na 43 na kuifanya timu hiyo kutoka kusini kuongoza kwa mabao 2-1 hadi mapumziko.
Kipindi cha pili, Simba SC iliendelea kupambana kutafuta matokeo na jitihada zao zilazaa matunda dakika ya 79 wakati Rushine De Reuck aliposawazisha kwa mkwaju wa penalti uliorejesha matumaini kwa mashabiki wa Msimbazi.
Wakiwa na kasi ya kusaka ushindi, Oura alikamilisha kazi yake nzuri dakika ya 88 kwa kufunga bao la tatu na la ushindi, na kuipa Simba SC pointi zote tatu muhimu katika dakika za mwisho za mchezo.
Ushindi huo unaendelea kuonyesha ushindani mkubwa wa ligi, huku Oura akidhihirisha umuhimu wake ndani ya kikao cha Simba SC kufuatia kiwango bora alichokionyesha.
