Simba Waishukia TFF Kisa Kauli za Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi

Simba Waishukia TFF Kisa Kauli za Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi
Simba Waishukia TFF Kisa Kauli za Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi

Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC imesema imesikitishwa na kauli zilizotolewa hadharani na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Klabu hiyo, ikieleza kuwa baadhi ya kauli hizo si sahihi na zimezua mkanganyiko miongoni mwa wadau wa Simba.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Novemba 15, 2026, Simba imesema Novemba 13, 2026 iliiandikia TFF barua rasmi kueleza msimamo wake kuhusu mwenendo wa mchakato wa uchaguzi, kutoa mapendekezo ya kuuboresha na kuomba uamuzi rasmi kwa maandishi.

Hata hivyo, Klabu hiyo imesema si sahihi kwa Kiongozi wa chombo kinachosimamia mpira wa miguu kujibu barua rasmi kupitia Vyombo vya Habari kabla ya kutoa majibu ya maandishi kwa Klabu.

Aidha, Simba imekanusha kauli zinazodai kuwa Klabu hiyo ina pande mbili zinazopingana, ikiwemo ofisi ya Mwekezaji iliyopo Masaki na ofisi ya Mwenyekiti Murtaza Mangungu iliyopo Msimbazi.

Related Posts