Nature

Jesca Magufuli Achukua Fomu Kuwani Ubunge

Jesca Magufuli ambaye ni Mtoto wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dr. John Pombe Magufuli, leo June 28 2025 amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa.

Jesca ni Binti ambaye amejipambanua kama sauti ya matumaini kwa Vijana na Wanawake wa Tanzania akisimamia maadili, haki na maendeleo jumuishi ambapo amelenga kupeleka nguvu mpya ya kijana Bungeni, kusimamia ajenda za maendeleo kwa Vijana, Wanawake na Jamii kwa ujumla huku akihakikisha UVCCM inasikika, inaonekana na inawakilishwa kwa heshima katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nipo tayari kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu, umoja na kwa kutanguliza maslahi ya Vijana na Wanawake, Geita inapeleka sauti ya mabadiliko chanya,” amesema Jesca Magufuli mara baada ya kuchukua fomu hiyo

ALSO READ | Paul Makonda Sasa Rasmi Vita na Gambo Ubunge Arusha

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *