Siku moja baada ya Singida Black Stars kufanya biashara ya kumuuza Josephat Bada kwenda JS Kabylie ya Algeria, habari njema kwa mashabiki wa timu hiyo ni kwamba uongozi umamelizana na kiungo Khalid Aucho aliyeitumikia Yanga kwa misimu minne ya mafanikio.
Bada ameitumikia Singida Black Stars kwa mkataba wa mwaka mmoja na kuipa mafanikio ambapo imepata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Chanzo cha kuaminika kutoka Singida Black Stars kimeniambia kuwa Aucho atakuwa mchezaji wa nne kutoka Yanga akiungana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Miguel Gamondi, baada ya Clatous Chama, Jonas Mkude Nickson Kibabage pia kutua kikosini hapo.

