Nature
Ole Sabaya Apigwa Chini Uteuzi CCM Arumeru, 6 Wateuliwa

Kauli ya Kwanza ya Ole Sabaya Baada ya Mchujo Kupita na Kukatwa

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amesema amekubaliana na uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM wa kuondoa jina lake kwenye orodha ya Wagombea ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi huku moyo wake ni mweupe na ametendewa haki na kwamba hatosusa wala kufikiria kuhama Chama bali atamuunga mkono Mgombea atakayepitishwa Jimboni kwake na Wagombea wengine wote nchini na ataenda kuwapigia kampeni na kumpigia kampeni Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili ashinde.

Akiongea kwenye mahojiano maalum kwa njia ya mtandao na Mwandishi Bakari Chijumba ikiwa ni mara yake ya kwanza kuongea tangu Wagombea watangazwe, Sabaya amesema “Kwakuwa kipimo cha moyo ni Mimi mwenyewe na sauti yangu nathibitisha na sauti hii kwamba moyo wangu ni mweupe nimetendewa haki, tulikubaliana wenyewe kutakuwa na demokrasia ndani ya Chama, hautakuwa mchakato wa Kiimla, demokrasia ni kupendekezwa na kutopendezwa kwahiyo hawakuniteua, nimekubaliana kwa moyo mweupe”

Alipoulizwa hatma yake ya kisiasa baada ya matokeo hayo, Sabaya amesema “Hapa ndio nimeanza nilikuwa napasha na nimeanza sasa kufanya siasa rasmi, nina miaka 38, Mimi asili yangu ni siasa , uongozi, asili yangu ni kuvusha na kuvusha Watu, nitaendelea na siasa, siasa ni kusaidiana Watu na kuwavusha kwahiyo hilo sitoliacha hadi maana hiyo itakapobadilika, Mungu bado yuko jiko anatengeneza vitu vyake bora kabisa, anatumia CCM, anamtumia Rais Dkt. Samia, Mungu anajua , bado ana sahani bora sana kwa ajili yetu, bado naamini Mungu anaifanya kazi yake na ataitoa ikiwa bora zaidi kuliko Mimi Binadamu nilivyoitegemea”

Related Posts