Nurdin Bilal Juma maarufu kama Shetta ( @officialshetta ) , Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ameibuka mshindi katika kura za maoni za chama hicho kwa nafasi ya udiwani Kata ya Mchikichini, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo unamuweka Shetta katika nafasi ya kuwa Mgombea Udiwani wa CCM kwa Kata hiyo kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano ya Oktoba 29, 2025.
Katika mchakato huo wa kura za maoni uliohusisha wagombea mbalimbali, Shetta akiwazidi wapinzani wake kwa kupata jumla ya kura 293 huku Azimkhan Akber Azmkhan akipata kura 178 na Joseph John Ngowa aliyepata kura 7 pekee.
Wilaya ya Ilala ina jumla ya kata 36, na Kata ya Mchikichini ni miongoni mwa kata zenye ushindani mkubwa kutokana na idadi ya watu na umuhimu wake katika jiji la Dar es Salaam.

