
Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro amethibitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho akichukua nafasi ya mtangulizi wake Balozi Emmanuel Nchimbi.
Dkt. Migiro ambaye amewahi kuwa Naibu-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anachukua nafasi hiyo baada ya Balozi Nchimbi kuchaguliwa na CCM kuwa mgombea mwanza wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Iwapo CCM itashinda kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu, Dkt. Nchimbi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
