
EQUATORIAL GUINEA: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha (NFIA), Baltasar Engonga amehukumiwa kifungo cha Miaka Minane jela pamoja faini ya Dola 220,000 (Tsh. Milioni 550) kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha za umma na kujitajirisha kinyume cha Sheria.
Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Mkoa wa Bioko nchini humo, ambapo Baltasar Engonga alituhumiwa kutumia fedha za umma kwa ajili ya matumizi yake binafsi, ikiwemo kutumia vibaya hela za safari na kutumia mamlaka yake Serikalini kuficha tuhuma za rushwa zinazomkabili.
Ikumbukwe Engonga aliingia kwenye vichwa vya habari Novemba 2024 baada ya kusambaa video takribani 400 za ngono akiwa na Wanawake tofauti.

