Nature

Mchezaji John Bocco, Alamba Shavu JKT Tanzania

Nahodha wa zamani wa Simba na Taifa Stars, John Bocco aliyekuwa akikipiga JKT Tanzania katika Ligi ya msimu uliopita, amelamba shavu jipya kwa maafande hao, licha ya kwamba hatakuwa na kikosi hicho katika Ligi Kuu msimu wa 2025-26.

Bocco aliyejijengea heshima akiwa na Azam FC aliyoipndisha Ligi Kuu mwaka 2007 na kutwaa nayo mataji kadhaa ikiwamo la Ligi Kuu 2013-2014 ilikuwa ikielezwa ni mmoja ya wachezaji watakaotemwa kwa kikosi cha msimu ujao cha JKT Tanzania, lakini jamaa bado yupo jeshini.

Tasrifa nilizopenyezewa ni kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 kwa sasa amebadilishiwa majukumu JKT Tanzania, kutoka kucheza uwanjani hadi kuwa kocha wa kikosi cha timu ya vijana cha U-20.

Taarifa hizo zinasema kuwa kwa msimu ujao unaotarajiwa kuzinduliwa Septemba 16, Bocco hatacheza tena akiwa na JKT badala yake atakuwa anakifundisha kikosi cha U-20 cha maafande hao wa Jeshi la Kujenga Taifa.

Related Posts