
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi amesema ni haki ya kikatiba kwa raia kusikiliza kesi, hivyo wasibuguziwe wale wanaofika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Akizungumza nje ya mahakama, Mwabukusi amesema:
“Sitaki sana kuzungumzia kile kinachoendelea ndani lakini ninachosema kikunwa utaratibu wa mahakama ya wazi hii sio ya kijeshi ni kiraia na raia wana haki ya kufika mahakamani na kusikiliza kesi na kama ukumbi ni mdogo wale wanaoweza kuingia ndani waingie kwa amani na wasikilize kwa amani kusiwe na viashiria vya Law inforce kwa mtu kujitutumua ukifikiri wewe una nafasi ya kipekee shauri linaposikilizwa mbele ya majaji wote ni sawa unayeshtaki na unayeshitakiwa nguvu ya ushahidi ndio inayotakiwa iongoze maamuzi ya mahakama,”.

