
Bilionea wa Nigeria na mfanyabiashara mashuhuri, Aliko Dangote, amefichua kuwa madereva wa malori katika shughuli za kiwanda chake cha kusafisha mafuta wanalipwa zaidi kuliko wahitimu wengi wa vyuo vikuu nchini humo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Nigeria, Dangote alisema: “Madereva wetu wanalipwa zaidi kuliko wahitimu. Ukiangalia wanachopata kwa mwezi ni karibu mara nne ya mshahara wa chini wa taifa.”
Ameongeza kuwa madereva wenye kumbukumbu safi ya miaka mitano bila ajali wanastahiki pia mikopo ya nyumba, hatua inayofanya kazi hiyo kuwa na mvuto mkubwa zaidi.

