
Klabu ya Azam Fc imetinga raundi ya pili ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kufuatia ushindi wa jumla wa 4-0 dhidi ya EL Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini Waoka mikate hao wakishinda 2-0 ugenini kabla ya kumaliza shughuli kwa ushindi wa 2-0 nyumbani Azam Complex, Chamazi.
Azam Fc watachuana na KMKM Fc ya Zanzibar kwenye raundi ya pili, KMKM ikifikia hatua hiyo kufuatia ushindi wa jumla wa 4-2, ushindi wa 2-1 ugenini kabla ya kushinda 2-1 nyumbani.
FT: Azam FC 🇹🇿 2-0 🇸🇸 EL Merriekh Bentiu (Agg. 4-0)
⚽ 16’ Yoro
⚽ 90+3’ Saadun
