
Kufuatia madai yaliyotolewa na ndugu wa Humphrey Polepole kupitia mitandao ya kijamii Jeshi la Polisi limeeleza kuanza kufuatilia tuhuma hizo.
Leo Oktoba 6, 2025 imeenea video ya mtu mmoja aliyejitambulisha kama Agustino Polepole aishie Denmark akidai mdogo wake ametekwa usiku wa kuamkia leo.
Jeshi la Polisi katika taarifa yake limeeleza pia kuwa linamsuburi Polepole kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

