Nature

Mwanamke Akiri Kumuua Mumewe na Kumzika Chumbani Kwao Huko Geita

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Martha Japhet (44) mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Mzalendo Kijiji cha Mawemeru, Kata ya Nyarugusu wilayani Geita kwa tuhuma za mauaji ya mume wake aitwaye Shabani Paschal (55) mkulima na mchimbaji madini.

Tukio hilo limebainika Oktoba 16, 2025 katika Kitongoji cha Mzalendo baada ya taarifa hizo kufikishwa kituo cha polisi ikielezwa kuwa Shaban hajaonekana nyumbani kwake tangu Oktoba 11, 2025 majira ya saa 3:00 usiku.

Jeshi la Polisi limesema baada ya kupokea taarifa hiyo lilifanya uchunguzi na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Martha kwa ajili ya mahojiano, ambapo mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa alimshambulia mume wake kwa kutumia kitu chenye ncha kali sehemu ya kichwani.

“Baada ya kugundua kuwa amefariki, alichimba shimo ndani ya chumba walichokuwa wanalala, akamzika, akajaza kifusi cha udongo kisha kuweka magunia ya mihogo juu yake ili kuficha ushahidi,” imesema taarifa.

Related Posts