
Mwimbaji wa Bongofleva kutokea Bad Nation Label, Marioo amesema atayaweka hadharani majina ya mastaa wote wakubwa wanaomtongoza mpenzi wake Paula.
“Kipindi mpenzi wangu alikuwa na ujauzito, walitokea wajuaji wengi wakamshawishi aitoe ile mimba kwa sababu pengine mimi nisingemfaa. Tena wengi ni hawa hawa watu maarufu mnawajua.”
“Nashukuru mpenzi wangu hakuweza kufanya hivyo na mimi nikapuuzia.
Yakaendelea maisha, na sasa hii ndiyo busara yangu ya mwisho kwa wadada na wakaka wa mjini — watu maarufu, wanasiasa, machawa na makuwadi”.
“Naenda kuwa na tabia ya kuwaanika hadharani wote ambao mnanitumia meseji za kimalaya kila siku, mnaong’ang’ania kutaka kumuunganisha au kujaribu kumtongoza mke wangu mtarajiwa.
“NITAWAUMBUA WOTE bila kujali status zenu. Chats zenu ninazo na kila siku anaonyeshwa. Msione anacheka na nyie, yaone mazee mazima ovyo ovyo!”.
“Na wote mliokuwa mnamupa ushauri wa kipumbavu baada ya post yangu ya jana — wote kawarudisha, yaani kimsingi wote mpo kama mnavyozaliwa.” – Marioo.

