
Nakatiza mitaa ya Makumbusho. Vibarabara vimenyooka lami tupu na vifremu. Bidhaa za kike nyingi zaidi kuanzia vipodozi, viatu, nguo za nje na za ndani. Zile za ndani ndani ndo nyingi zaidi. Kila mtaa ni pisi tu kwa kwenda mbele.
Njoo Dar ndio uulize kwanini mimi sijajenga mbwa wewe. Wanaume hatujaumbiwa uchoyo kwa hawa viumbe uzao wa Eva. Natumiaje pesa yangu kivyangu kama tenki la “brevisi’? Toto mbili tatu za geti au za kona ‘dei tu dei’ ndio maisha yetu.
Daslama ina totozi nyie nyie nyie. Acheni tu! Nilienda Rwanda ‘lasti wiki’, wanasifiwa tu, ila warembo wapo Dar. Pisi za Kinywarwanda hazina pozi. Hazina swaga wala mikato. Zote zinafanana kama sare za magereza. Ndo nini?
So huwezi kupata fleva kwa pisi zinaofanana nchi nzima. Ndiyo maana Wachina, Wajapan hata wafilipino na Wakorea. Hawana mvuto kwa sababu hii. Kufanana! Ukija Dar kuna Wachina, Wakorea, Wahindi hadi Waperuvian. Wewe tu
Ukitaka pisi nyeupe nenda kitaa cha Singidani kwa ‘Ofisho Nai’ au Arachuga kwa Wameru na wale Wambulu. Ukitaka ngozi laini na mahaba nenda Tangaaa. Ukitaka kabati, burudoza na mabode byulda ni Mbeya, Tabora, Kagera na Simiyu.
Singida wana bifu na miguu tu ila kwingine mashalah. Arachuga ya Wameru na Wambulu wana bifu na meno, mengine alhamdulilah. Na Tabora ni wachache saaaana wanaofikishana uzeeni kama vile ‘tugeza izi wani’. Mtatemana tu.
Mbeya hawana shida yoyote ila inategemea na ‘profesheno’ yake. Kama mtu wa tungi wana undugu wa kukesha baa. Kama ni mtu wa maombezi tegemea mikesha ya kanisani. Akiwa ‘bizinesi wumani’ tegemea kukesha safarini. Wao wanajituma kuliko masela wao.
Kagera hawana mambo meeengi. Ila lazima uwe mtu wa kijikweza kweza. Pisi za kitaa cha Kagera hazitaki ujinga wa kujishusha na kujitilisha huruma. Unatakiwa mtu ambaye ukiwa na laki moja keshi, umvimbie hata Arapisii kama siyo Arasiii.
Umewahi kufakamia pisi kali ya Kikurya? Acha kabisa kuna ‘taimu’ nilihisi Mungu alianza kuziumba pisi za Kikurya kabla ya Wangindo na Wayao. Tulaani tabia za vipigo vya kaka zao, lakini ni kama wana sababu za msingi vile? Tru!
Raha ya pisi za Kikurya ni adabu, heshima na uvumilivu. Adabu ni kama kobe, heshima kama benz na uvumilivu kama trekta. Mtoto wa Kikurya akionywa jambo na mume hata kama mume kafariki. Bado ataendelea kuheshimu agizo hilo.
Kuna pisi za Kichaga. Ukikutana nazo zile ‘ojiii’ za kutoka Kilema, Kibosho, Marangu mtoni ndani ndani. Katikati ya tendo anaweza kustopisha. Wao hawaoni hatari kuomba teni ili aongeze miguno. Wana ‘dieniei’ na pesa na hujivunia hilo.
Suala la pesa kwao lina baraka za kimila. Usije na njaa zako ukataka pisi za Vunjo, Boma Ng’ombe na Siha. Ukitambulishwa swali lao la kwanza ni “Ana hela? Pesa ni kila mtu anazo ila hela ni wachache wenye nazo. Ndio wanavyoamini.
Kila kabila lina swaga na mikato yake. Lakini wakiwa hapa Dar ni laini moja, wanavua ukabila na utamaduni wao. Wanakuwa ni Wadaslama na wananata na biti la ‘kitauni tauni’. Na wawapo hapa Dar umri wao hauzidi miaka 30 kila mwaka.
Kwa mwaka wana ‘besidei’ kibao pindi wapatapo bwana mpya au pesa za ghafla. Majina hubadilika na kutambulika kwa jina lake la Insta. Hawataki Insta kutumia jina halisi la Anamaria, anataka aitwe ‘Cute Ane’ yaani ‘ofishocuteane’.
Kiasi kikubwa madem wa kanda ya kati. Walijenga undugu rasmi na rangi nyeusi. Lakini ukienda Insta hugeuka kuwa waarabu au wafilipino. Madem wa Insta wote weupe pee tena ngozi laiini kama sufi. Kutana naye uso kwa uso.
Wakija Dar wote wanakula misosi ya baa. Hawawezi kupika geto wala kusuuza vyombo. Wakiingia geto ni kulala na kuamka mambo mengine anamaliza dada wa kazi. Inategemea na dada mwenyewe wa kazi. Wengi ni kitega uchumi pia.
Yaani dem anatoka zake Mwanza na kutimba Dar. Akipata ukonki masta, naye anafanya ‘skautingi’ ya pisi ya mkoani na kuileta Dar. Kabla haijamasta inakuwa dada wa kazi. Ushamba ukimtoka naye anaingia mzigoni kudanga.
Naye anafanya ‘skautingi’ yake na kuleta vipaji vipya vya kudanga mjini. Wanabebana kuletana Dar kwa kazi maalumu isiyo na leseni wala ithibati. Kimsingi wanatumia mtaji mwili waliopewa bwerere na Muumba wa Mbingu na Nchi.
Ukizama ndani sana utagundua hii Daslama haina mwenyewe. Ni chimbo la yeyote yule mradi uwe mjanja tu. Tazama vilabu vikubwa havina kiongozi mwenyeji wa Dar wote wamekuja. Bosi wa mkoa ni wakuja, madisii na maarapisii ni wakuja.
Zamani mikoani wangejua mtu aliyetoka Dar kwa kiswahili tu. Lakini hivi sasa ni ngumu sana kusikiliza kiswahili cha Masanja Mkandamizaji kama kipimo cha mkazi wa Daslama. Ni kwamba Dar ya sasa ni ya wote wenyeji hawapo.
Ili kujua swaga za makabila na mikato yao lazima utembee. Siyo utoke Kawe kwenda Kitunda ili ukajue tabia za Wakurya. Na siyo utoke zako Kimara kwenda Keko ili ukajue tabia za Wanyakyusa. Ni lazima uende kwenye mikoa yao.
Makabila yaliyojazana hapa Dar hayana swaga za kwao. Hunata na Udaslama kuanzia tabia hadi majina. Katika hali ya kawaida unaweza kuamini kwamba Gigy Money ana asili ya Mwakaleli ndani ndani? Huwezi kuamini hilo kwa sababu ana Udaslama ojii.

