
Baada ya taarifa kutoka shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kutoka kuhusiana na kusitisha mkataba wa aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), nikasema nimtafute kocha wetu bhana Hemed Suleiman maarufu Kwa jina la “Morocco” ili nijue Kwa niaba ya wengine pengine ni nini kimepelekea shirikisho hilo kusitisha mkataba wake.
Taarifa ya TFF imesema kuwa wao wamesitisha mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote mbili, lakini Cha ajabu baada ya kuzungumza na kocha Morocco alisema kuwa nanukuu
“hata mimi nimeona taarifa hizo mitandao kama mlivyoona ninyi na sina taarifa yoyote kuhusiana na mimi kufutwa kazi, Kwa sababu utaratibu huwa tunapewa taarifa kwa njia ya maandishi lakini kwangu imekuwa tofauti, Kwa kifupi sina taarifa rasmi” mwisho wa kunukuu.

