Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amejikuta katika wakati mgumu mitandaoni baada ya kupoteza zaidi ya wafuasi 50,000 kwenye akaunti yake ya Instagram ndani ya masaa 24 pekee.
Kwa mujibu wa takwimu za mtandaoni, jana Diamond alikuwa na takribani wafuasi 18.8 milioni, lakini leo idadi hiyo imeshuka hadi kufikia takriban 18.7 milioni.
Hata hivyo, sababu rasmi ya kupungua kwa idadi hiyo kubwa ya followers bado haijafahamika, na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakijadili tukio hilo kwa namna tofauti, wengine wakisema huenda linatokana na mabadiliko ya tabia za watumiaji wa mitandao au “system cleanup” ya Instagram.
Mpaka sasa, Diamond Platnumz bado hajaweka wazi chochote kuhusiana na tukio hilo.

