Nature

TFF Bado Wana Mpango na Kocha Morocco, Wamfanyia Jambo Hili

KAMA ulidhani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtupa aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, basi unakosea kwani ameandaliwa mpango mzito.

Taarifa kutoka TFF zinasema, licha ya Morocco kutolewa katika nafasi hiyo ya kuinoa Stars, shirikisho hilo litampeleka nje ya nchi kuongeza ujuzi zaidi

Kiongozi huyo wa TFF amenieleza kuwa, sio Morocco peke yake, wapo makocha wengine ambao watapata fursa hiyo ya kwenda kujiendeleza zaidi kisha kuja kupewa timu za taifa hapo baadaye

“Msione kama Morocco ametupwa, hapana…bado tunakwenda kumuendeleza zaidi, tutamtafutia kozi za kwenda kusoma Ulaya, ili baadaye arudi kwenye majukumu haya haya.

“Morocco atakuwa wa kwanza tu, lakini huu ni mpango endelevu, kuna wenzake wengine watafuata au kuungana naye huko, mchakato huo umeshaanza na unafanyiwa kazi na idara ya ufundi ya TFF,”

Related Posts