Kuna kipindi nilifikiri ndoa yangu imefika mwisho. Mimi na mke wangu tulianza maisha kwa upendo mkubwa, tukifanya kila kitu pamoja. Tulikuwa marafiki, wapenzi, na washirika wa kweli.
Lakini miaka michache baadaye mambo yalibadilika ghafla. Mke wangu alianza kujitenga, akawa mkali, na akapoteza kabisa hamu ya kushughulikia majukumu ya nyumbani. Nilianza kuhisi kama ninaishi na mtu asingaye nijali.
Kila siku nilirudi nyumbani nikikuta nyumba haijasafishwa, chakula hakipo, na watoto wakijilaza njaa. Nilihisi kuchanganyikiwa. Nilipojaribu kuzungumza naye, alinijibu kwa hasira, akisema amechoka na hajui kwa nini kila kitu kimekuwa juu yake. Nilijaribu kumfariji, lakini kadri nilivyojitahidi, ndivyo tulivyozidi kuwa mbali.
Nilihisi kama upendo wetu unayeyuka taratibu. Wakati mwingine nilikaa sebuleni nikiangalia picha zetu za zamani tulivyokuwa tunacheka, kusafiri, na kupanga ndoto zetu. Sasa nyumba ilikuwa kimya, imejaa huzuni na ukimya wa maumivu.
Nilianza kujiona kama sina maana tena kwake. Marafiki walinipa ushauri wa kuachana naye, lakini moyoni nilijua bado nampenda. Nilihitaji suluhisho, si vita. Soma zaidi hapa

