Nature

Tundu Lissu Aweka Pingamizi Kwa Mashahidi wa Kificho

Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti @chadematzofficial Tundu Lissu imeahirishwa kwa muda mpaka Msajili wa Mahakama atakapopanga ratiba kwani kesi hiyo inasikilizwa kwa vipindi (sessions).

Kesi hiyo imeahirishwa baada ya Lissu kuwasilisha hoja mahakamani hapo akipinga chumba ambacho aliwekwa shahidi P11 ambaye ni shahidi anayelindwa (shahidi wa kificho) ambapo chumba hicho kingetumika na mashahidi wengine pia wanallindwa.

Mbele ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Lissu alisema sababu za yeye kupinga chumba hicho ni kwamba hakuna shahidi yeyote ambaye kwa amri ya ulinzi iliyotolewa na mahakama anatakiwa kuwa kwenye ‘kiboksi’, wote waliopewa ulinzi wanatakiwa kutoa ushahidi wao kwenye kizimba cha kutoa ushahidi.

Lissu ameeleza kuwa shahidi anatakiwa kukaa kwenye eneo ambalo ataonekana na Jaji au Hakimu pekee bila kuonekana na watu wengine. Hata hivyo Lissu anesema chumba kilichopo mahakamani jaji hawezi kumuona shahidi pindi kesi inapoendelea.

Pamoja na hayo ameieleza mahakama kuwa sheria inayotumika kuwalinda mashahidi haijakidhi vigezo vya kuwa sheria kwa kuwa haikuchapishwa katika gazeti la serikali kama ambavyo inapaswa. Amefafanua kuwa tafiti zimefanyika katika maktaba ya taifa, bungeni na hata ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakuna sehemu ambapo sheria hiyo ikichapishwa.

Sababu nyingine ni kuwa amri iliyowahi kutolewa na Jaji Mtembwa kuwa Jaji anayeendesha kesi inayowahusu mashahidi wa siri anatakiwa kupewa majina ya mashahidi hao na kuwafahamu lakini katika kesi hii majaji hawajapewa taarifa hizo, huku akitahadharisha kuwa katika kesi hii mashahidi wanajulikana na Jamhuri pekee.

Sababu nyingine ni kuwa endapo Jamhuri itahitaji kutumia kizimba maalum italazimika kuiomba mahakama lakini katika kesi hii Jamhuri haikuomba.

Baada ya kuieleza mahakama hoja zake hizo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga uliiomba mahakama kupata muda wa kutosha kujibu hoja za Lissu kwani zinahitaji majibu ya kisheria na kitafiti

Related Posts