Muda mfupi baada ya Baraza la Mawaziri kutangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan huku jina lake likikosekana kwenye mkeka mpya, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika ujumbe ufuatao:
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipindi tulichopata kuwatumikia watanzania katika nafasi mbalimbali.
Naomba kumshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu, mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fursa adimu uliyonipa katika vipindi mbalimbali kuwatumikia watanzania. Naomba nikuahidi tutaendelea kuunga mkono juhudi na maono mazuri ya uongozi wako pamoja na Serikali ya Awamu ya 6 unayoiongoza. @samia_suluhu_hassan
Naomba pia kuwashukuru wananchi na matajiri wangu wananchi wa Jimbo la Karagwe kwa ushirikiano na imani kwangu. Sasa nimepata muda wa ziada wa kukaa jimboni ili kazi iendelee na kwa kasi zaidi.
Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.

