TMA Yatoa Tahadhari ya Mvua Kwa Mikoa Hiii

Kulingana na TMA, hali ya hewa inatarajiwa kuwa tofauti katika mikoa mbalimbali:

Mikoa ya Njombe na Ruvuma yatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache, pamoja na vipindi vifupi vya jua.

Mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma, Rukwa, Iringa, Songwe, Mbeya, na Morogoro (Kusini) yatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache, pamoja na vipindi vya jua.

kuwa na mawingu kiasi na mvua katika maeneo machache, pamoja na vipindi vya jua.

Mikoa ya Singida, Dodoma, Pwani (ikiwemo Visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Morogoro (Kaskazini), na Tanga yatarajiwa kuwa na mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache, pamoja na vipindi vya jua.

Mikoa ya Manyara, Arusha, na Kilimanjaro yatarajiwa kuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Visiwa vya Unguja na Pemba vitatarajiwa kuwa na mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache, pamoja na vipindi vya jua.


TMA imeto angalizo kuhusu uwezekano wa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo machache ya Mikoa ya Ruvuma na Njombe. Wakaazi na watembelea wa maeneo hayo wanashauriwa kuchukua tahadhari zinazohitajika.


Kwa siku ya Ijumaa tarehe 21 Novemba 2025, TMA inatarajia mabadiliko kidogo tu ya hali ya hewa ikilinganishwa na leo.

Kwa upande wa joto, miji mbalimbali inatarajiwa kufikia viwango tofauti vya joto. Kwa mfano, Dar es Salaam na Dodoma zitarajiwa kufikia nyuzi joto 33, huku Arusha ikiwa na nyuzi joto 29 na Njombe 24. Joto la chini kabisa litahisi Njombe kwa nyuzi 11, na joto la juu zaidi litakuwa Dar es Salaam, Dodoma na Tabora kwa nyuzi 33.

Upepo kwenye maeneo ya pwani unatarajiwa kuvuma kutoka upande wa Kaskazini Mashariki kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa. Hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi.

Taarifa hii imetolewa na Ofisi ya Taifa ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo, tarehe 19 Novemba 2025.

Related Posts