Nature

Boyeli Awatangazia Vita Kina Dube, Ataka Kiatu Cha Ufungaji Bora Ligi Kuu Bara

MALENGO YANGU NIKUWA MFUNGAJI BORA KWENYE MASHINDANO YA CAF

Mshambuliaji wa Yanga SC, Andy Boyeli, amesema moja ya malengo yake makubwa katika msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni kuchukua kiatu cha ufungaji bora (CAF Golden Boot).

Akizungumzia mchezo wa kesho dhidi ya FAR Rabat, Boyeli amesema anaingia uwanjani akiwa na matumaini, ari na malengo binafsi ya kufanya makubwa, huku akisisitiza kuwa hana sababu ya kushindwa kufikia rekodi ambayo iliwahi kuwekwa na aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele.

“Malengo yangu ni kuchukua kiatu cha ufungaji CAF. Kama Mayele aliweza, kwa nini mimi nishindwe? Ninaamini uwezo wangu na najiandaa kutoa zaidi kwa timu,” amesema Boyeli.

Boyeli ameongeza kuwa muda mwingi amejiweka vizuri kimwili na kiakili ili kuhakikisha kila nafasi anayoipata anaigeuza kuwa mabao, huku akiahidi mashabiki wa Yanga kuona kiwango kikubwa zaidi msimu huu.

Related Posts