Nature

Rais Samia “Baada ya Maridhiano Katiba Mpya Itafuata”

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema suala la Katiba mpya lipo palepale na kwamba kwa sasa anasubiri Tume ya kuchunguza matukio ya October 29 imalize kazi kisha ataunda Tume ya maridhiano na baada ya hapo mchakato wa Katiba mpya utaanza.

Akiongea na Wazee wa Dar es salaam leo December 02,2025, Rais Samia amesema “Tutasimama na kuilinda nchi hii kwa nguvu zote, yaliyopita sindwele tugange yajayo, kama madai ya wenzetu ni Katiba hakuna aliyekataa kurekebisha Katiba ya nchi hii, niliunda Tume ya haki jinai wakaniletea wanayoyaona Watanzania, ya muda mfupi na wa kati mengi tumeyatekeleza lililobaki la muda mrefu la Katiba tulisema tutalitekeleza, na nimesema tuunde Tume ya
maridhiano kisha litafuata la Katiba, mnaendaje kuunda Katiba wakati wote kila Mtu kavimba mashavu Katiba ipi itaundwa hapo?”

“Kwasababu wamechafua nchi nimeunda Tume kuchunguza vurugu, nimewapa miezi mitatu, kisha Tume ya maridhiano itafuata kisha tutaunda Katiba, hakuna aliyekataa, leo wanasema wameingia barabarani wameharibu nchi wanadai Katiba, Katiba ipo wapi?, inaning’inia wapi tuipachue tuwape?, Katiba ni mchakato”

Related Posts