Nature

Mufti Abubakary Zuber Afunguka “Tuache Matamshi ya Uchochezi”

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakary Zuber ameviomba vikundi mbalimbali kutoka kwenye dini zote viache kutoa matamshi ambayo yataleta mhemko na uchonganishi kwa wafuasi wa dini zao.

Mufti Zuberi ameyasema hayo wakati akitoa tamko lake mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es salaam ambapo amewaomba Viongozi wa vikundi vya Kidini waache malumbano ya kidini, badala yake wahamasishe wafuasi wao kuiombea nchi amani na utulivu.

“Mimi kama kiongozi Mkuu wa dini ya Kiislam naviomba vikundi vya dini zote, viache kutoa matamshi ambayo yataleta mhemko kwa wafuasi wao pamoja na wa dini nyingine, na waache malumbano ya kidini, badala yake yahamasishe wafuasi wao kuiombea nchi yetu amani na utulivu.”

Aidha Mufti Zuber amesisitiza ya kuwa vitabu vya Mungu vya dini ya Kiislamu vinawataka kuishi na watu wote kwa wema “Mungu ametuambia kwamba hatukatazwi sisi kuishi na wasiokuwa Waislam kwa wema na kwa kuwa hayo ndio maisha ambayo tumechaguliwa na Mungu kuishi na kwa kuzingatia moja ya mambo ambayo tumekubaliana kuwa maisha ya watu ni lazima yalindwe kwa gharama yoyote.”

Related Posts