Simba na Azam FC ndio klabu zilizotoa wachezaji wengi wanaounda kikosi cha Taifa Stars kitakacho cheza fainali za AFCON 2025 nchini Morocco! Klabu hizo kila moja imetoa wachezaji sita [6].
Yanga inafatia kwa klabu zilizotoa wachezaji wengi wanaounda kikosi cha Stars kitakacho cheza AFCON 2025 ikiwa imetoa wachezaji wanne [4].
Singida Black Stars yenyewe imetoa wachezaji watatu [3] na kukamilisha orodha ya klabu zilizo toa wachezaji zaidi ya mmoja kwenye kikosi cha Taifa Stars kuelekea fainali za AFCON 2025.
