Nyota watatu wa @yangasc wapo katika wakati mgumu kusalia kwenye timu hiyo, Andy Boyeli, Shadrack Isaka Boka na Muossa Balla Conte wote tia maji tia maji katika dirisha dogo la usajili.
Kocha Pedro ameweka wazi orodha ya Nyota anaokusudia kubaki nao huku kukiwa na urejeo wa beki wa Kimataifa wa Ivory Coast, Yao Koassi Atoula aliyekua majeruhi ambapo mwanzo mwa msimu huu aliongeza mkataba wa miaka miwili huku akiwa nje ya kikosi kutokana na Majeraha.
Aidha Uongozi wa Yanga Afrika unatazamia kuongeza nyota wawili wa Kitanzania katika eneo la Ulinzi wa kushoto kama backup ya Mohammed Hussein Zimbwe Shabalala na Mshambuliaji mmoja kama muendelezo wa kuandaa mbadala wa Clement Mzize mwakani na kiungo wa kati kama mbadala wa Balla Conte.
