Mshindi wa Bahati Nasibu Avaa Kinyago Familia Isimtambue

Mwaka 2019, mwanaume mmoja nchini Jamaica aliyefahamika kwa kifupi cha jina A. Campbell alizua gumzo kubwa baada ya kusaini ushindi wa Jamaica Super Lotto akiwa amevaa vazi la kutisha. Lengo lilikuwa kuficha utambulisho wake dhidi ya familia na watu wa karibu.

Campbell alishinda dola za Jamaica milioni 158, lakini alisubiri kwa siku 54 kabla ya kujitokeza kuchukua hundi yake kwenye Hoteli ya Spanish Court, Kingston. Alieleza kuwa alikumbwa na hofu, msongo wa mawazo na wasiwasi kuhusu shinikizo la watu pamoja na hatari za kiusalama endapo angejitokeza wazi.

Nchini Jamaica, ni jambo linaloonekana mara kwa mara kwa washindi wa bahati nasibu kutumia barakoa au mavazi ya kujificha ili kulinda faragha na usalama wao. Kwa Campbell, ushindi huo umefungua ukurasa mpya wa maisha, akiwa na mipango ya kununua nyumba, kuwekeza na kujenga mustakabali wake.

Tukio hili lilibaki kuwa somo kwa wengi: wakati pesa zinaweza kubadilisha maisha kwa ghafla, faragha na usalama ni utajiri usiopimika.

Related Posts