Kocha Mkuu wa klabu ya Raja Casablanca kutoka nchini Morocco Fadlu Davids, ameonesha nia ya kuhitaji huduma ya beki wa kati wa klabu ya Simba Rushine De Rueck baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Kwa upande wa mmiliki wa mchezaji huyo anaonekana yupo tayari kwa deal hilo huku akiweka wazi kuwa Simba yupo kwa mkopo wa mwaka mmoja tu ambao hauna kipengele cha kuongeza.
Katika hatua nyingine pia kocha huyo anahitaji huduma ya kiungo wa kati Jean Ahoua raia wa Ivory Coast pamoja na winga hatari raia wa Congo DR Elie Mpanzu Kibisawala.
Wachezaji hao inaonekana kuwa itakuwa rahisi kuwang’oa Simba kwakua kocha huyo ameanza kuijenga vizuri Raja Casablanca na wanatamani wamtimizie matakwa yake.
Ifahamike kuwa Fadlu Davids amejiunga na Raja Casablanca mwanzoni mwa msimu huu kutoka katika klabu ya Simba ambako alitimka mapema tu.
Simba kazi kweli kweli😪
