Harmonize na Kajala Wamerudiana Bwana, Kuvalishana Pete Upya


STAA wa filamu nchini, Kajala Masanja imedaiwa kesho Jumatatu atavishwa pete ya uchumba kwa mara nyingine na Harmonize ambaye ni supastaa wa Bongo Fleva.

Chanzo chetu cha habari kutoka kwa Harmonize kimedai, kesho jioni Kajala atavishwa pete hiyo ndani ya meli.

“Habari ni hii, kwa sasa penzi la Kajala na Harmonize limerudi upya kwa kasi, hivi ninavyokwambia kesho anavishwa pete ya uchumba na baada ya hapo ndoa haitachukua muda mrefu. Safari hii pete havishwi hotelini, anavishwa katika meli na shughuli itahidhuriwa na watu wachache,” kilisema chanzo hicho.

Jana Jumamosi, Desemba 27 , Harmonize anayetamba kwa sasa na wimbo wa ‘Leo’ aliyomshirikisha Mbosso, aliweka wazi kuwa yupo tayari kumvisha pete tena mpenzi wake huyo Kajala Masanja.

Hayo aliyaandika kupitia ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni siku moja imepita tangu wawili hao warudiane upya.
“Nikianza kuzungumza kuhusu mpenzi wangu, upendo wa maisha yangu, sitoweza kumaliza leo! Lakini pia siwezi kukaa kimya. Wala siwezi kulichukulia poa suala la yeye kuja kwenye shoo YANGU. Nilifurahi sana kukuona tena mahali pangu pa kazi.


“Nikianza kuzungumza kuhusu mpenzi wangu, upendo wa maisha yangu, sitoweza kumaliza leo! Lakini pia siwezi kukaa kimya. Wala siwezi kulichukulia poa suala la yeye kuja kwenye shoo YANGU. Nilifurahi sana kukuona tena mahali pangu pa kazi.

“Tumepitia mengi na sasa tumekuwa kama ndugu. Kwenye jina langu kuna jina lako, na kwenye jina lako kuna jina langu. Dunia nzima inafurahia kwa ajili yetu. Endapo mkono wako utanipokea, nitaweka pete kwenye kidole chako tena, na milele. Tuanzie upya (RESTART),” ameandika Konde

Harmonize na Kajala waliweka wazi kurudiana kwao Desemba 25, 2025 Visiwani Zanzibar ambapo Konde alikwenda kufanya shoo.


Hii itakuwa ni mara ya pili wawili hao kuvishana pete, kwani ikumbukwe Juni 25, 2022, Konde alimvisha pete katika tukio lililofanyika hoteli ya Serena na kulipa jina la ‘Late Lunch’, huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwamo uongozi wa Lebo ya Konde Gang, Mkurugenzi wa TVE, Francis Chiza ‘Majizzo’, Aunty Ezekiel, Martin Kadinda na wengineo.

Aidha, licha ya kuvishana pete penzi hilo lilivunjika miaka miwili iliyopita na kila mmoja akafuata njia yake.
Lakini sasa wameibua tena mjadala kutokana na mabusu waliyopigana katika shoo ya Konde iliyofanyika Zanzibar. Huku kukiwa na tetesi kuwa wawili hao walirudiana tangu Mei mwaka huu.

Related Posts