Uongozi wa mchezaji Aziz Ki umetoa ufafanuzi Rasmi Kuhusu mtoto Wake Kufariki…

Uongozi wa mchezaji Stephane Aziz Ki umetoa ufafanuzi rasmi kufuatia taarifa zilizosambaa zikidai kuwa mtoto wa mchezaji huyo amefariki dunia.

Kupitia taarifa rasmi, uongozi huo umeeleza kuwa mtoto aliyefariki hakuwa mtoto wa Aziz Ki, bali alikuwa mtoto wa dada yake, ambaye alifariki dunia nchini Burkina Faso akiwa kazini.

Taarifa hiyo imekuja baada ya jumbe nyingi za pole kutolewa na mashabiki, klabu mbalimbali pamoja na wadau wa soka walioguswa na taarifa za awali.

Uongozi wa Aziz Ki umeeleza kuthamini upendo, maombi na mshikamano uliooneshwa na jamii ya soka, huku ukiomba heshima na faragha kwa familia katika kipindi hiki kigumu.

Mwisho, uongozi huo umeomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na kuipa familia nguvu na faraja.

Diva Media Africa

Related Posts