AFCON 2025: Sahau 16 bora, haya ni mafanikio mengine 5 ya Tanzania

Kwa mara ya kwanza katika historia yake ya ushiriki wa AFCON, Tanzania (Taifa Stars imevuka hatua ya makundi na kuingia 16 bora. Hilo peke yake tayari ni habari kubwa. Lakini kwa macho ya uchambuzi wa kina, kufuzu huku ni sehemu ndogo tu ya simulizi pana zaidi kuhusu mabadiliko ya Taifa Stars katika soka la Afrika.

Kwa miaka mingi, Tanzania imekuwa ikipewa nafasi ya “mshiriki” badala ya “mshindani” kwenye mashindano makubwa. Ilikuwa timu inayokuja kujifunza, kukutana na wakubwa, kisha kuondoka mapema. AFCON 2025 imebadilisha kabisa taswira hiyo. Sio tu kwa matokeo, bali kwa namna timu imecheza, imehimili presha, na imejijengea utambulisho mpya.

Kundi C lilikuwa gumu, Nigeria yenye historia na ubora wa kudumu, Tunisia iliyozoea hatua za mtoano, na Uganda jirani anayefahamiana vyema na Tanzania kwa mazingira ya soka la Afrika Mashariki.

Ndani ya muktadha huo, Tanzania haikuonekana kama timu ya kuleta ushindani, bali kama mshiriki anayekuja kujifunza na kujiandaa kwa ajili ya michuano ijayo, lakini akapata mabao bila ushindi, akakusanya alama kwa sare mbili, na hatimaye akafuzu 16 bora kupitia nafasi ya mshindi wa tatu bora wa kundi C. Ilishindwa kufanya hivyo mwaka 1980, 2019 na 2023.

Soma zaidiLakini hata baada ya shangwe za kufuzu 16 bora hilo ni muhimu na jambo moja tu, lakini kuna masuala kadhaa zaidi ya mafanikio yanayostahili kuangaliwa. Kwa kuondoa hisia na kuangalia takwimu, historia na mwelekeo wa timu, AFCON 2025 imeacha alama tano muhimu zinazothibitisha kuwa Taifa Stars ipo kwenye njia ya mabadiliko ya kweli.

Kwa mara ya kwanza, Tanzania imemaliza kundi katika nafasi ya tatu. Kihistoria, hili ni jambo kubwa zaidi kuliko linavyoonekana.

Mwaka 1980, Tanzania ilimaliza ya mwisho kwa alama moja. Mwaka 2019, ilimaliza ya mwisho bila alama. Mwaka 2023, tena ilijikuta mkiani kwa alama mbili. AFCON 2025 imevunja mfululizo huo wa kumaliza mkiani, na kuonyesha kuwa Taifa Stars sasa inaweza kushindana kwa alama, si kwa heshima pekee.

Nafasi hii ya tatu pia imeleta Tanzania kwenye mjadala wa kisasa wa AFCON, mfumo wa ”best third-placed teams”, timu zinazoshika nafasi ya tatu na kusonga mbele. Mataifa kama Benin na hata Ivory Coast, mabingwa watetezi wa zamani, waliwahi kutumia njia hii kufika hatua za juu. Tanzania sasa ipo kwenye ramani hiyo ya kimkakati ya mashindano haya.

Related Posts