Nature

Aggrey Mwanri Achukua Fomu Kugombea Ubunge SIHA “Umri Sio Kikwazo”

Aliyewahi kuwa Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Balozi wa Pamba nchini Bw. Aggrey Mwanri leo Jumamosi Juni 28, 2025 amechukua fomu ya kuomba kuidhinishwa na Chama Cha Mapinduzi CCM, ili kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge kwenye Jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro.

Mwanri mwenye umri wa 69, amezungumza na Vyombo vya habari Mara baada ya kuchukua fomu hiyo akisisitiza kuwa Umri kwake sio tatizo kwani Bungeni hawaingii watunisha misuli ama wapiganaji na kusisitiza kuwa bado yupo imara na akili inafanya kazi kwa ukamilifu wake.

“Mimi nimejenga uzoefu na ambao utawasaidia vijana wanaotaka kuwania uongozi, ukiwa katika nafasi kama hizi unahitaji kufundisha, unahitaji kulea, unahitaji kusimama na kuonesha namna ya kuongoza na kule tunakoenda. Bungeni hatupeleki Tyson, Bungeni tunapeleka mtu ambaye kichwa kinatwanga. Ukienda pale ukasimama, hatuangalii misuli. Tunapeleka mtu ambaye anawasilisha maendeleo na matumaini ya wananchi wake.” Amesema Mwanri.

Katika maelezo yake pia amewataka wananchi kupuuza baadhi ya taarifa mitandaoni zinazodai kuwa hatogombea, akisema taarifa hizo ni potofu na kujitokeza kwake leo kuchukua fomu ni dhihirisho la dhamira yake ya kutaka tena kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro.

Wakati wa uchukuaji fomu hiyo, Mwanri aliambatana na Mkewe

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *