
Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema mechi ya Dabi ya Kariakoo ndio mechi za Simba za kuonesha ubora wake walionao katika kikosi chao.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutua Dar es salaam Ahmed Ally amesema wametua muda huo huo na wanaelekea visiwani Zanzibar kwaajili ya Maandalizi ya Dabi ya Kariakoo.
Klabu ya Simba itakuwa ugenini kucheza mchezo wa ligi Kuu dhidi ya Yanga, Mchezo huo utachezwa March 1 katika uwanja wa New Amaan Complex majira ya saa 2:15.
