Al Ahly imerejea kileleni mwa Kundi B kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji, AS Far Rabat, wakifikisha alama 4 baada ya mechi mbili sawa na Young Africans Sc iliyoshuka mpaka nafasi ya pili.
AS FAR Rabat iliyopoteza 1-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Wananchi ipo nafasi ya tatu alama moja baada ya mechi mbili huku JS Kablie iliyopoteza 4-1 dhidi ya Al Ahly kwenye mechi ya kwanza ikiburuza mkia alama moja baada ya mechi mbili.
Kwingineko, Mamelodi Sundowns imetoshana nguvu na MC Alger ya Algeria kwa sare tasa huku Sundowns ikikwea kileleni mwa Kundi C alama nne baada ya mechi mbili huku MC Alger ikiwa nafasi ya tatu alama moja baada ya mechi mbili.
FT: AS FAR Rabat π²π¦ 1-1 πͺπ¬ Al Ahly
β½ 37β Bouriga
β½ 68β Trezeguet
FT: MC Alger π©πΏ 0-0 πΏπ¦ Mamelodi Sundowns
MSIMAMO KUNDI B
- πͺπ¬ Al Ahly β mechi 2β pointi 4
- πΉπΏ Yanga Sc β mechi 2β pointi 4
- FAR Rabat β mechi 2β pointi 1
- JS Kablie β mechi 2β pointi 1

