Nature

Ali Kamwe Ampa Maua Yake GSM “Miaka Minne Nyuma Yanga Ilikuwa Haitamaniki”

Ameandika Haya Ali Kamwe

GSM. GSM. GSM. Asante sana.

Asante Sana Ghalib Said Mohammed kwa kuifanya @yangasc Yetu ifike ilipofika Leo hii kwenye ramani ya mpira Barani Afrika.

Miaka minne tu iliyopita, Yanga yetu ilikuwa inatupa unyonge kila ulipoanza mjadala unaohusu Ligi ya Mabingwa Afrika. Tulikaa miaka 25 sisi bila mechi ya Group Stage.

Lakini tazama Leo, October 26, 2025, Young Africans Sports Club imekuwa KLABU YA KWANZA TANZANIA kufuzu HATUA YA MAKUNDI YA CAF CHAMPIONS LEAGUE MARA 3 MFULULIZO.

Asante sana GSM.

Tunajua hupendi sana Sifa hizi, hupendi sana kuwa mbele, Wewe sio BILIONEA kama wale wengine, Wewe ni mtu Mkimya, Mstaarabu, mwenye huruma, mkweli na Upendo wa kweli na Klabu yetu

Tunajua hupendi tutambe sana kuhusu wewe, Lakini kwa Leo naomba utuvumilie na ukubali asante yetu.. Sisi @yangasc Tunasema ASANTE NA TUNAJIVUNIA SANA WEWE

Jana, Tulipokuona Uwanjani, wewe pamoja na Familia yako, mioyo ya Wanayanga ilikuwa na amani na imani kuwa Jambo Umelivalia njuga.

Tunajua ugumu wa mechi ya jana, wavimba macho hawakupenda kabisa Tuweke hii rekodi. Walitamani tuwe kama wao, walifanya kila hila, Lakini ALHAMDULILLAH ..

Mipango ya Mungu ikashinda. Tukafuzu GROUP STAGE YA LIGI YA MABINGWA mara 3 mfululizo. Sio kinyonge Wananchi👊🏼

Tulisema tunatengeneza Msingi imara wa Kimataifa na Mwanga unaonekana. Wengine safari yao ilikuwa ingia Toka. Leo Ligi ya Mabingwa, Kesho Shirikisho.. Rekodi ya kuunga unga sana🤩

Sisi @yangasc Tumechapa GROUP STAGE 3 MFULULIZO za LIGI YA MABINGWA AFRIKA .. Nasisitiza hapo, LIGI YA MABINGWA AFRIKAAA👊🏼

Asante sana GSM.

Tuna imani uwekezaji wako utakuwa Dira na nguvu Yetu kwenye Hatua ya Makundi msimu huu.👊🏼

Related Posts