Mnamo Agosti 1, 2025, Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe alimuoa mkewe Jasmin katika ndoa iliyofungwa jijini Arusha. Ndoa hiyo ilivuta hisia kubwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutokana na namna ilivyokuwa ya ghafla. Hata baba mzazi wa bwana harusi alikiri wazi kuwa hakuwa ameshirikishwa katika maandalizi ya ndoa hiyo. Hata hivyo, ndoa hiyo haikudumu sana, kwani katikati ya mwezi Septemba 2025, ilisambaratika rasmi, na hivyo ilidumu kwa takriban mwezi mmoja na nusu pekee.
Kwa upande mwingine, Suti Bega naye alifunga ndoa na mrembo wa kizungu mwenye asili ya Ufaransa mwanzoni mwa Disemba 2025. Hata hivyo, kufikia Disemba 31, 2025, ndoa hiyo ilikuwa imesambaratika, baada ya mke huyo kudai kuwa alipigwa na mume wake, jambo lililotajwa kama sababu kuu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo. Ndoa yao haikudumu hata kwa mwezi mmoja kamili.
Hali hizi mbili zimeacha gumzo kubwa kuhusu ndoa za watu maarufu na uhalisia wa maisha yao ya kifamilia. Kwa upande wako unadhani kwa nini ndoa za watu maarufu hazidumu?
