Jana ilikuwa siku ya kipekee kwa mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize ambaye alitangazwa kushinda tuzo ya goli bora la mwaka na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) katika usiku wa tuzo nchini Morocco.
Mzize ambaye hakuweza kufika mwenyewe akiendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni, alisema tuzo hiyo imemuongezea morali ya kuzidi kufanye vyema zaidi.
Mzize aliwashukuru wachezaji wenzake, makocha, viongozi na mashabiki waliomuungana mkono na kumpigia kura kwa wingi akitaja tuzo hiyo ni ya kila mmoja.
“Nawashukuru sana CAF kwa kunipa tuzo hii, naamini ni chachu kwangu, imeniongezea thamani na imeniongezea kitu kikubwa katika majukumu yangu”
“Nawashukuru pia wachezaji wenzangu kwa kuweza kupambana kupata tuzo hii, naamini hii ni tuzo yetu sote”
“Pia nawashukuru sana benchi la ufundi, viongozi na kipekee nawashukuru sana mashabiki kwa kunipigia kura na hatimaye kupata tuzo hii ya goli bora la msimu,” alisema Mzize

