Askari Trafiki Aliyeomba Rushwa Kwa Mzungu Mtalii Akamatwa na Polisi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limethibitisha kumkamata Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Mufindi anayefahamika kwa namba ya kazi WP.8402 CPL Bikusekela baada ya video inayomuonesha akifanya kitendo kibaya na cha utovu wa nidhamu akiwa kazini kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo Askari huyo tayari amechukuliwa hatua kali za kinidhamu kufuatia kitendo hicho ambacho kimekosolewa vikali na uongozi wa Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi limesema haliridhishwi na vitendo vya Askari wanaokiuka maadili na nidhamu ya kazi na limeonya kuwa halitasita kuchukua hatua kali kwa Askari yeyote atakayebainika kufanya vitendo vinavyochafua taswira ya Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla.

Related Posts