Nature
Baada ya Kukatwa CCM, Mpina Agonga Hodi ACT Wazalendo, Awagawa Wanachama

Baada ya Kukatwa CCM, Mpina Agonga Hodi ACT Wazalendo, Awagawa Wanachama

Saa za aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutua katika Chama cha ACT-Wazalendo zinahesabika, baada ya kiongozi huyo kubisha hodi huku akieleza kuwa yuko tayari kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais, Jambo TV imedokezwa.

Uamuzi huo wa Mpina, ambaye ameondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa na CCM kuwania Ubunge wa Kisesa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni misimamo yake ya kuikosoa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu, unatajwa kuwagawa viongozi wa ACT-Wazalendo. Baadhi yao wanahofia misimamo hiyo, huku wengine wakieleza kuwa anapaswa kupewa jukwaa hilo.

Katikati ya mjadala huo juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, inadaiwa kumeibuka upinzani mkubwa ndani ya chama, huku viongozi wakionesha kutokuwa tayari kumsimamisha kwenye nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa mbunge huyo wa zamani haendani na aina ya siasa ya chama hicho.

Mpina anasifika kwa siasa ngumu zenye kujikita katika kuikosoa serikali kwa ukali, tofauti na utamaduni wa ACT-Wazalendo unaosifika kwa kufanya siasa za masuala na ujenzi wa hoja.

Taarifa za Mpina kujiunga na ACT-Wazalendo zimechagizwa zaidi na taarifa za kuongezwa muda kwa watia nia wa nafasi ya ubunge ndani ya chama hicho. Katibu Mkuu, Ado Shaibu, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza juu ya chama hicho kuongeza muda, pasipo kufafanua zaidi ni katika nafasi gani.

Wakati kukiwa na mvutano juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, baadhi ya wanachama waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika chama na Baraza Kivuli la Mawaziri, akiwemo Mwalimu Philbert Macheyeki, wamesikika wakieleza kuwa Mpina ni turufu kubwa ya kukijenga chama hicho na kukipatia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Macheyeki amesema kuwa hadi sasa chama hicho kimewatangaza watia nia wawili katika nafasi ya urais—Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Aroon Kalikawe—na kwamba ujio wa Mpina utakuwa ni chachu zaidi kwa ajili ya mafanikio ya chama chao.

“Luhaga Mpina amejizolea sifa za kuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Awamu ya Sita na kinara wa kuibua kashfa mbalimbali nzito za ufisadi…

Related Posts