Nature

Baba Levo Amtishia Nyau Zitto Kabwe “Saa Tano na Nusu Nitakuwa Nimeshachukua Jimbo Kigoma Mjini”

Msanii Clayton Revocatus Chipando Maarufu kama Baba Levo leo Agost 24,2025 akiongea na waandishi wa habari ameushukuru Uongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Kwa kumuamini kwenda kugombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini.

Baba levo amekiri katika mchakato wa kuwania kiti cha Ubunge anatarajia kwenda kupata Upinzani kwa Zitto Kabwe ambaye anawania Ubunge kupitia Chama cha ACT Wazalendo

“Ninaamini naenda kukutana na upinzani na mmoja kati ya mpinzani ambao nategemea kukutana nao atakuwa ni Zitto Zuberi Kabwe nikasema nitumie mic hizi kumtahadharisha kwamba muda umefika watu wa Kigoma Wanaamua sasa ni yeye achague aje ili nimshinde adharirike au akimbie”

Aidha,Baba levo amewaomba Wananchi wa Jimbo la Kigoma Mjini Kujitokeza kwa Wingi katika zoezi la Kupiga ili aweze kupata Ushindi Mkubwa ambao utaleta mabadiliko Jimboni hapo

Related Posts