Nature
Baba Levo Chali Kura za Maoni Kigoma, Shabani Ng’enda Ashinda

Baba Levo Chali Kura za Maoni Kigoma, Shabani Ng’enda Ashinda

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini anayetetea nafasi yake, Shabani Ng’enda, ameibuka mshindi katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 2,168.

Clayton Revocatus Chipando maarudu kama BabaLevo ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,080, huku Mwandishi wa Habari Baruani Muhuza akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 264.

Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM kwa Jimbo la Kigoma Mjini, Sadick Kadulo ambaye pia ni Katibu wa chama hicho Wilaya ya Kigoma.

  1. Kirumbe Shabani Ng’enda – kura 2,168
  2. Clayton Revocatus Chipando, Baba Levo– kura 2,080
  3. Baruani Muhuza – kura 264
  4. Dkt. Ahmad Yahya Sovu – kura 247

Related Posts