Nature

Benson Kigaila: Si Lazima Mbowe Kwenda Mahakamani Kesi ya Tundu Lissu

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Bara, Benson Kigaila ameeleza kuwa si lazima kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe kushiriki vikao vya CHADEMA kwasababu yeye ni mwanachama wa kawaida.

Akizungumza na Wilberforce Ngoto @wilberforcengoto8218 wa kipindi cha Maswali na Majibu kinachorushwa na Jambo TV, Kigaila amesema kuwa mwanachama wa kawaida wa CHADEMA hushiriki mkutano mkuu wa tawi kwenye tawi lake.

Aidha ameeleza kuwa Mbowe amekuwa akifanya mambo kwa ajili ya CHADEMA bila kujionesha ikiwamo kuwasiliana na kumuona Mwenyekiti wa chama hicho taifa Tundu Lissu gerezani, likiwa ni jibu kwa baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa wakihoji kutoonekana kwa Mbowe katika viunga vya mahakama kufuatilia kesi zinazomhusu Lissu na CHADEMA.

Related Posts