Bibi wa Miaka 70 Asombwa Maji, Akivuka mto

Bibi wa Miaka 70 Asombwa Maji, Akivuka mto
Bibi wa Miaka 70 Asombwa Maji, Akivuka mto

Bibi mwenye umri wa miaka 70, ambaye jina lake bado halijajulikana amefariki dunia, kwa kusombwa na maji ya Mto Mkondoa.

Imeelezwaa kuwa Bibi huyo alikuwa anajaribu kuvuka eneo la Kidete Stesheni.

Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amesema mvua hizo zilizonyesha tangu Machi 9 mwaka huu,pia zimesababisha mafuriko na kuathiri makazi ya wananchi katika maeneo ya Miyombo, Mhenda na Mkata Stesheni.

Amesema tathmini ya awali inaonesha zaidi ya nyumba 100 katika eneo la Miyombo zimeingiliwa na maji ya mafuriko, huku Serikali ikiendelea kufuatilia hali ya Mto Mkondoa ambao kina cha maji kinaendelea kuongezeka na kuleta hofu ya kuathiri zaidi makazi ya wananchi.

Related Posts