Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeijibu Simba SC kufuatia malalamiko yao kuhusu uhamishaji wa mchezo wa Kariakoo Derby.
Kwa mujibu wa barua hiyo, Young Africans SC (Yanga) ndio wenyeji wa mchezo husika, na walipewa taarifa na wamiliki wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa siku ya derby kutakuwa na matumizi mengine ya uwanja huo.
Kutokana na hali hiyo, Yanga waliiomba TPLB kuruhusu mchezo uchezwe katika Uwanja wa New Amaan Complex. Bodi ya Ligi imeeleza kuwa ombi hilo lilikubaliwa kwa kuwa uwanja huo ulikuwa tayari umekaguliwa na kupitishwa na Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF.
Aidha, TPLB imesisitiza kuwa Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, hana kosa lolote kwa kutoa taarifa hiyo, kwani mchakato wa maamuzi ulikuwa umeidhinishwa rasmi na mamlaka husika.
