
Ameandika Bondia Hassan Mwakinyo Kupitia Instagram:
Ningeomba niombe radhi kwa wote watakao kwazika na ujumbe wangu huu kwa MH Rais na unisamehe pia MAMA YANGU kama kijana wako nimezungumza kwa hasira, hisia au maumivu…MH RAIS tunafaham ya kua wewe ni mtu mwema sana na ni platform kubwa ya taifa letu lakini wapo baadhi ya watu wako wanatumia nafasi ya uwongozi wako kutuletea maisha ya kinyonge na uonevu watu wengine kwa kigezo cha kwamba ni watu wako.au ume watuma MH RAIS wengine tunakutazama wewe kama keki ya TAIFA na haipaswi kuwepo watu wafanye tukuone uko kwa ajili ya watu flani tu ambao wanatumia nafasi ulizo wapa kwa uwongozi wako kukandamiza jitihada za wengine wanyonge. sababu ya chuki tu.
Kwa siku nyingi nimekua na vita kubwa ya chini chini na mtu mmoja ambae kwa sasa anatumia nafasi ya uwongozi wako kunikwamisha sana anatumia jina lako kwenye mamlaka nyingi kama umemuagiza kufanya anayofanya ikiwemo kukwamisha jitihada zangu binafsi kwa makusudi I’m tired of this mimi ni kijana mpaambanaji mwenye ndoto kubwa na sehemu pekee binaadam anaweza kuongea ni pale akichoka kuvumilia sikusudii kuchochea wala kukosea yoyote lakini nimechoka kuvumilia na haya yanayo endelea na hawa watu ambao kwa namna flani wanakuharbia MH @samia_suluhu_hassan 🙏🏽

