Nature

Bonge la Dada Akataa Shilingi Milioni 3 ya Bure….

Dansa maarufu Bongo, Bonge la Dada (Queen Fraison) amesema amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa baadhi ya wanaume wanaodhani wanaweza kumpata kimwili.

Amedai aliwahi kupigiwa simu na kuambiwa nenda sehemu fulani kachukua Sh3 milioni ya bure ila akakataa!.

“Alisema nikachukue milioni 3, nikauliza ya nini akasema wewe chukua tu… Wewe si mzima, jiongeze,” amesema na kuongeza.

“Nilikataa maana sipendi fedha za bure, nataka nipate fedha kwa kufanya kazi. Nipate fedha kwa kucheza (dance),” ameeleza Bonge la Dada.

Ikumbukwe hivi karibuni Bonge la Dada ambaye ni dansa wa Mbosso, alijizawadia gari katika birthday yake.

Related Posts