Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) linajiandaa kumsimamisha kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Thiaw, kwa muda mrefu kufuatia utovu wa nidhamu uliotokea katika mchezo wa hivi karibuni.
Thiaw anakabiliwa na rungu hilo baada ya kufanya uamuzi wa utata wa kuiondoa timu yake uwanjani (kutoa timu), kitendo ambacho ni kinyume na kanuni na taratibu za mashindano ya kimataifa. Ingawa Tume ya Nidhamu imethibitisha kuwa adhabu hiyo itakuwa ya muda mrefu, idadi kamili ya mechi atakazokosa bado haijawekwa wazi hadi taratibu za kisheria zitakapokamilika.
Tukio hili limezua mjadala mpana katika soka la Afrika, likija wakati ambapo CAF, chini ya uongozi wa Dr. Patrice Motsepe, imekuwa ikisisitiza kuimarisha nidhamu na kufuata kanuni kwa mataifa yote wanachama. Kusimamishwa kwa Thiaw kutaacha pengo kubwa katika benchi la ufundi la “Simba wa Teranga” (Senegal) wakati wakijiandaa na michuano ijayo, huku wadau wa soka wakisubiri tamko rasmi la CAF ili kujua hatima ya kocha huyo ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timu hiyo hivi
