BREAKING; Tanzania Yafuzu Hatua ya 16 Bora AFCON 2025

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars hatimae kwa mara ya kwanza katika historia inafuzu kucheza hatua ya 16 bora ya AFCON 2025 baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Tunisia na kumaliza nafasi ya tatu kwenye kundi lake na kufuzu hatua ya mtoano kupitia mfumo wa playoff.

Tanzania anafuzu kwa Playoff akiwa ameambatana na Timu zingine zilizofuzu katika nafasi ya tatu bora katika makundi yao ni Msumbiji, Benin na Sudan.

Angola alikuwa anaiombea Tanzania ipoteze leo ili apate nafasi ya playoff ila sasa wamefungana kwenye alama 2 na Tanzania na utofauti wa magoli -1 ila Tanzania anafuzu kwa kufunga magoli mengi 3 dhidi ya Angola aliyefunga mawili.

Hii ni mara ya nne Tanzania inashiriki AFCON 1980, 2019, 2023 na hizo zote ilikuwa inaishi makundi, sio mbaya kwenda kama best looser hata Bingwa mtetezi (Ivory Coast) alienda kama best looser 2023 😃

Related Posts